Afueni kwa wazazi wizara ikisema hisabati na sayansi sio lazima Sekondari Pevu

0

SERIKALI imefanunua kwamba haitakuwa lazima wanafunzi wa Gredi 10, 11, na 12 kusoma masomo hisabati na sayansi.

Badala yake wanafunzi hao wana uhuru wa kuchagua masomo wanayotaka kulingana na uwezo na matamanio yao.

Wizara ya Elimu imetangaza kuwa kutakuwa na uhuru wa wanafunzi kuchagua masomo wanayotaka kufanya wanapofika shule za sekondari pevu baada ya kukamilisha sekondari msingi.

Kwanzia mwaka ujao wanafunzi wa Gredi ya 9 watajiunga na sekondari pevu kulingana na masomo watakayochagua ikiwemo Sayansi, Spoti, (Sayansi jamii, Sanaa na spoti, na Sayansi ya Tekinolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM).

“Haitakuwa lazima kwa wanafunzi wa Gredi 10, kuchagua somo la Sayansi wala Hisabati. Watoto wana uhuru wa kuchagua maosmo wanayotaka, tusiwalimbikizie masomo,” alifafanua Katibu wa Elimu Dkt Belio Kipsang.

Hata hivyo alisisitiza kuw ani sharti shule zote nchini kuchagua masomo ya sayansi na hesbati ili kuongeza idadi ya wataalam wa tajriba hiyo.

Hii ni afueni kwa wanafunzi hao ambao wazazi wao walianza kuuliza maswali kwanini wanalazimika kuchukua masomo hayo ilhali wanapenda masomo mengine kama spoti.

Lakini kwenye mahojiano ya kipekee na Taifa Leo, Katibu huyo wa Elimu alisema mfumo wa CBC inalenga kumpa mwanafunzi nafasi bora ya kufana kwenye masomo ambayo anapenda tofauti na mtaala wa 8-4-4 ambao masomo ya Hisabati na Sayansi ni lazima.

Serikali iliandaa mdahalo wa elimu kutathmini safari hiyo iliyoanza miaka tisa iliyopita. Wanafunzi wa kwanza wa CBC wamefika Gredi ya Tisa.

Katibu huyo alisema Jopokazi la Rais la kuthathmini Elimu nchini, lilipendekeza kuwa asilimia 60 ya shule zote za sekondari ya juu zinafaa kuwa na masomo ya sayansi na hesabati.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mombasa Prof Laila Abubakar, ambaye alikuwa kwenye jopokazi, hilo alisema ni sharti shule zote ziwe na masomo ya sayansi na hesabu.

“Lakini si lazima wanafunzi wachukue au wachague masomo hayo. Mwanafunzi anaweza kuchagua sporti na afane maishani,” alieleza Prof Abubakar kwenye mdahalo wa elimu.

Mwenyekiti wa muungano wa wazazi nchini Bw Silas Obuhatsa, aliwasihi wazazi kuhudhuria mdahalo huo unaoendelea kote nchini ili kutoa maoni yao kuhusu mtaala.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *