Maswali Mudavadi, Weta wakikwepa kurasmishwa kwa ndoa ya kisiasa ya Ruto na Raila

0

MKUU wa Mawaziri Musalia Mudavadi na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula,  waliwaacha  wengi na maswali kwa kukwepa kuhudhuria mkutano wa kutiwa saini mkataba wa maelewano kati ya vyama vya United Democratic Alliance (UDA) na ODM jana katika ukumbi wa KICC.

Wawili hao ni vinara wenza waanzilishi wa muungano wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Rais Ruto.

Hii ni licha ya kwamba chama chake za zamani Amani National Congress (ANC) kuungana rasmi na UDA kwa lengo la kukipa nguvu chama hicho kinachoongozwa na Rais William.

Kufuatia hatua hiyo, iliyofanikishwa Januari 17, 2025, aliyekuwa kiongozi wa ANC Gavana wa Lamu Issa Timamy aliteuliwa kuwa mmoja wa manaibu kiongozi wa ANC huku aliyekuwa Katibu Mkuu Omboko Milemba akipewa wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu wa UDA.

Lakini jana, baada ya kuhudhuria mkutano wa Kundi la Wabunge wa Kenya Kwanza (PG) katika Ikulu ya Nairobi, Bw Mudavadi hakufika KICC kushuhudia kutiwa saini mkataba wa UDA na ODM.

Shughuli hiyo ilipokuwa ikiendelea KICC, Mkuu huyo wa Mawaziri alikuwa katika kaunti ya Kakamega kuhudhuria Ibada ya shukrani katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Friends’.Kabla ya kusafiri kwa helikopta hadi Kakamega, Bw Mudavadi alimpokea Balozi wa Hungary Zsolt Meszaros afisini mwake Nairobi.

“Leo, Ijumaa nimempokea Balozi wa Hungary Zsolt Meszaros aliyenitembelea afisini mwangu. Tumejadili nafasi za kuwezesha kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili haswa katika nyanja za biashara, elimu na kawi,” ikasema taarifa fupi kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii X.

Hata hivyo, Bw Milemba, ambaye ni mbunge wa Emuhaya, alifika KICC kushuhudia kutiwa saini kwa mkutaba huo wa ushirikiano kati ya ODM na UDA.Mawaziri Kipchumba Murkomen (Usalama) na mwenzake wa Leba Alfred Mutua ni miongoni mwa viongozi wengine waliofika kushuhudia kitendo hicho cha kihistoria.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *