Taharuki yatanda Gusii Stadium Raila akizomewa na wakazi

0

HALI ya taharuki imetanda katika uwanja wa Gusii huku sehemu ya vijana wakimzomea Kiongozi wa ODM Raila Odinga, siku mbili baada ya kutia saini mkataba wa kushirikiana na Rais William Ruto.

Bw Odinga anahudhuria kuzinduliwa kwa jezi mpya za timu ya Shabana ambayo inacheza kwenye Ligi Kuu ya FKF.

Vijana katika sehemu mbali mbali za uwanja walianza kuwika “Raila Must Go” kwa Kiswahili “Raila Aende” huku wengine wakiimba “Haki Yetu”.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga alipowasili katika uga wa Gusii katika hafla ya kuzinduliwa kwa jezi mpya za timu ya Shabana FC. Picha|Wycliffe Nyaberi

Baadhi ya mashabiki walimkosoa Bw Odinga kwa matamshi aliyotoa Alhamisi akiwa katika Kituo cha Mafunzo ya Wakulima cha Kisii ambapo alipuuzilia mbali azma ya aliyekuwa Waziri Fred Matiang’i kuwania urais 2027.

Vijana waliimba “Matiang’i! Matiang’i” kwa Gavana Simba Arati kila alipotaja jina la Raila Odinga.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *