Bunge La Taifa La Uganda Kufungwa
Bunge la taifa la Uganda litafungwa kuanzia mwezi Juni mnamo tarehe 28 mpaka Julai tarehe 11 kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.
Karani wa bunge hilo la Uganda Jane Kibirige amesema hatua hiyo itatoa fursa kwa majengo ya bunge kunyunyuziwa dawa.
Hatua hii inajiri juma moja tu baada ya kamati ya bunge la serikali ya Uganda kutangaza kuwa zaidi ya wafanyakazi wake mia moja wameambukizwa virusi vya corona.
Ni juma moja lililopita ambapo raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni aliyatangaza masharti mapya zaidi ya kuthibiti maambukizi pamoja na msambao wa covid 19 katika taifa hilo ukiwamo kusitishwa kwa safari za ndege na kuifunga mipaka yake.
- Mpaka sasa, ni takribani watu sabini na watatu elfu, mia nne na mmoja waloambukizwa virusi vya corona na idadi ya waloiagadunia kutokana na virusi hivyo ni mia saba kumi na wanane.