Bunge La Taifa La Uganda Kufungwa

Bunge la taifa la Uganda litafungwa kuanzia mwezi Juni mnamo tarehe 28 mpaka Julai tarehe 11 kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Karani wa bunge hilo la Uganda  Jane Kibirige  amesema hatua hiyo itatoa fursa kwa majengo ya bunge kunyunyuziwa dawa.

Hatua hii inajiri juma moja tu baada ya kamati ya bunge la serikali ya Uganda kutangaza kuwa zaidi ya wafanyakazi wake mia moja  wameambukizwa virusi vya corona.

Ni juma moja lililopita ambapo raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni aliyatangaza masharti mapya zaidi ya kuthibiti maambukizi pamoja na msambao wa covid 19 katika taifa  hilo ukiwamo kusitishwa kwa safari za ndege  na kuifunga mipaka yake.

  1. Mpaka sasa, ni takribani watu  sabini na watatu elfu, mia nne na mmoja waloambukizwa virusi  vya corona na idadi ya waloiagadunia kutokana na virusi hivyo ni mia saba kumi na wanane.
Share with Your Friends