Ufadhili Wa Elimu Kwa Wanafunzi nchini Kenya
Waziri wa wizara ya elimu profesa George Omore Albert Magoha kwa sasa anakariri kwamba hakuna haja ya kuwepo hofu kuhusu swala zima la maambukizi ya virusi vya corona katika shule za hapa nchini.
Magoha anasema visa vichache vya virusi vya corona ambavyo vimeripotiwa katika baadhi ya shule nchini vitashughulikiwa katika huku wahusika wakitengwa pasi na kusababisha hali ya taharuki miongoni mwa wazazi, walimu na wanagenzi.
Akinena katika eneo la Manyatta gatuzi la Kisumu ambako leo hii anafuatilia kwa ukaribu mchakato mzima wa wanagenzi kupewa ufadhili wa mpango wa elimu yetu kujiunga na shule za sekondari.
Magoha aidha amesisitiza kuwa mpango huo ambao serikali inautekeleza kwa ushirikiano na benki ya Equity inaendeshwa kwa usawa na wala hamna mapendeleo yoyote kabisa.