Ufadhili Wa Elimu Kwa Wanafunzi nchini Kenya

Waziri wa wizara ya elimu profesa George Omore Albert Magoha kwa sasa anakariri kwamba hakuna haja ya kuwepo hofu kuhusu swala zima la maambukizi ya virusi vya corona katika shule  za hapa nchini.

Magoha anasema visa  vichache vya virusi vya corona ambavyo vimeripotiwa katika  baadhi ya shule nchini vitashughulikiwa katika huku wahusika  wakitengwa pasi na kusababisha hali ya taharuki miongoni mwa wazazi, walimu na wanagenzi.

Akinena katika eneo la Manyatta gatuzi la Kisumu ambako leo hii anafuatilia kwa ukaribu mchakato  mzima wa wanagenzi kupewa ufadhili wa mpango wa elimu yetu kujiunga  na shule za sekondari.

Magoha aidha amesisitiza kuwa mpango huo ambao serikali inautekeleza kwa ushirikiano na benki ya Equity inaendeshwa kwa usawa na wala hamna mapendeleo yoyote kabisa.

 

 

Share with Your Friends